Jamvi la KiswahiliMashairi

MGENI KIPOFU

(Picha kwa hisani ya MuseumNext)

 

Na Abdul S. Shaban

 

Tazama bila ya hofu, hapo ndipo utaona,
Alosema muongofu, alitazama kwa kina,
Pasinapo hitilafu, mimi naye naungana,
Kuwa mgeni kipofu, hata kama anaona.

Mgeni huwa kipofu, hata kama anaona,
Vitu vyenye upotofu, hasemi atauchuna,
Huwa anaudhohofu, mjuvi kuonekana,
Kweli mgeni kipofu, hata kama anaona.

Hata aone mnofu, nayo pilau imefana
Huku njaa takatifu, mgeni imembana,
Kusema ni ualifu, japo aona bayana,
Haki mgeni kipofu, hata kama anaona.

Mwisho ninawaarifu, wa juzi, leo na jana,
Muone na msadifu, wala hamtabishana,
Zaidi utamsifu, mjumbe wake Rabbana,
Haki mgeni kipofu, hata kama anaona.

Invo

Invo

The online involvement editor manages this author. The articles posted are associated with the various writers and editors for the involvement Newspaper.

One thought on “MGENI KIPOFU

  • Samuel

    Mmmh kweli mgeni kipofu hata kama anaona

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *