Involvement

USICHEZEE BAHATI

 

Na ABDUL SHABAN

{abdoolmtyro@gmail}

 

Wewe si mzuri sana, punguza kuniringia

Wazuri nimewaona, sura zao zavutia

Na mengi wewe hauna, ila nimewakimbia

Moyo umekuchagua, kwako ni kama bahati.

 

Wangapi wamenitaka, watukufu wa tabia

Warembo waloumbika, wakiniona hulia

Nawakataa hakika, ni kwako nakimbilia

Moyo wangu waugua, nimekupenda banati.

 

Nimesema nakupenda, si vyema kuninunia

Wenzako wananiganda, mapenzi kuyalilia

Nawe waleta mapozi, bahati imekujia

Uache kunizingua,usichezee bahati.

 

Sina nyumba wala mali,ni mbora wa tabia

Nina mapenzi ya kweli, si kwamba najisifia

Ila najua kujali, kutunza kuhudumia

Juu yako kuchagua, sijesema ya laiti.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top