Involvement

SHAHARI YA RAMADHANI

NA ABDUL SHABAN

{abdoolmtyro@gmail.com}

Shahari ya Ramadhani, inatubishia hodi, inataka kuandama,
Inayo ziso kifani, fadhila, sada na sudi, pamoya na takirima,
Basi tuipokeeni, na huku zetu fuadi, zashasha na kuterema,
Ni mwezi ulo na shani, ameamuru Wadudi, ufungwe wote mzima,
Ni faradhi tufungeni, kufunga hatuna budi, sisi tulo isilama,
Ikiwa tu waumini, wa kweli kwake Wahidi, hino funga ni alama,
Mwezi mwandamo jamani, tuuzinge kwa juhudi, katika duniya nzima,
Tisaa wa ishirini, shabani ndiyo miadi, jioniwe tuwe wima,
Ukioneka angani, siku ya pili hubidi, tuamke na swauma,
Usipooneka sini, tutatimiza idadi, ili iwe ni khatima,
Shaabani thalathini, bila punjo na kuzidi, tumwa wetu ashasema,
Kwa ajili ya Manani, tufunge tujijadidi, kumcha Mola Qayyuma,
Funga ni ibada hini, ilotukufu zaidi, ‘meiteua Karima,
Piya ni kinga makini, maovu huyasharidi, katika yetu mitima,
Basi tujitoleeni, kumridhisha Swamadi, kwa kufanya yalomema,
Funga na tuifungeni, tunali yake kusudi, hapa nafunga kalima,
Natusisingizieni, maradhi yaso shadidi, na matumbo kutuuma,
Kufunga tusiat’eni, tuche siku ya waidi, na moto wa jahanama,

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top