Na Wangu Kanuri
kanuriwangu@gmail.com
Oktoba 12 mwaka wa 2019 ni siku ambayo daima itakuwa kumbukumbu kwani mwanariadha Eliud Kipchoge amevunja rekodi aliyokuwa amejiwekea ya kukimbia kwa kilomita arubaini na mbili kwa muda wa saa moja na dakika hamsini na tisa.
Isitoshe jina lake limeandikwa katika kitabu cha rekodi cha dunia cha Guiness. Eliud aliyekuwa amejibidisha na kuamini kuwa ataweka historia duniani, aliwafanya wakenya wengi kujumuika kumtizama akivunja rekodi hii iliyofahamika kama INEOS 159.
Rais Kenyatta aliwaongoza wakenya katika kumhimiza Kipchoge kulenga lengo lake huku naibu wake mheshimiwa Ruto na bibiye wakisafiri Vienna kumpa mkono anapokimbia.
Kusudio kuu lake Kipchoge lilikuwa kuonyesha kuwa hakuna pingamizi lolote iwapo mtu anataka kuwa wa kwanza katika lolote. Isitoshe, alisisitiza kuwa hashindani na wengine bali anashindana na muda na kuweka historia katika dunia.
Shindano hili liliokuwa likitizamwa moja kwa moja katika mitandao, limewafunza watu kuwa; shindano letu si dhidi ya marafiki, maadui ama wenzetu bali dhidi ya muda. Pili, mbio yetu yapaswa kuwa dhidi ya lengo tulizojiwekea na mwishowe mbio yetu ni katika tunayonuia kulenga.
Eliud Kipchoge vilevile amesema kuwa alikuwa mwenye tumbo joto baada ya kupokea simu kadha wa kadha kutoka viongozi wakuu katika serikali ya Kenya ikiwemo rais Kenyatta. Hata hivyo, bado alishikilia msimamo wake dhidi ya kuweka rekodi ya wanariadha duniani.
Akizungumza baada ya shindano hilo, Kipchoge amesema kuwa imemchukua mwanadamu miaka sitini na tano kuweka historia katika mbio za dunia kwa hivyo yeye amejazwa na furaha ghaya kuweza kuifufua historia hii. Mwenyekiti wa INEOS bwana Jim Ratcliffe alisema kuwa hakuamini vile Kipchoge alikimbia mtawalia mbio ya kwanza kwa muda wa chini ya saa moja.