Involvement

Matokeo ya Ligi kuu ya Mabingwa Barani Ulaya

Na Dennis Mungai

Raundi ya pili za mechi za Ligi kuu barani Ulaya zilikamilika leo kukiwa na matokeo za kushangaza. Newcastle United, ambayo walirudi katika michuano hii baada ya miaka ishirini, waliwaadhibu Paris St Germain mabao manne kwa moja. Ulikua mshindi kubwa kabisa katika historia ya klabu hiyo katika michuano hii. Mechi zingine zilizochezwa siku ya Jumatano ni ikiwemo Borussia Dortmund kutoka sare tasa dhidi ya AC Milan. Barcelona walishinda Porto 1-0 nayo Lazio kuchapa Celtic 2-1.

Foden, Alvarez na Jeremy Doku waliifungia Man City na kuhakikisha ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya RB Leipzig kabla ya kucheza na Arsenal siku ya Jumapili. Atletico na Shaktar walipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Feynoord na Antwerp mtawalia. Siku ya Jumanne mchezaji wa Arsenal Bukayo Saka alipata jeraha huku timu yake ikipigwa mabao mawili kwa moja na Lens.

Masaibu ya Manchester United yaliendelea baada ya kupoteza mechi nyingine nyumbani Old Trafford. Rasmus Hojlund alifungia United mabao mawili lakini hayakutosha kuzuia kupigwa kwa timu yake 3-2 na Galatasaray. Wilfred Zaha, mchezaji wa kitambo wa United, alifungia Galatasaray huku Casemiro akionyeshwa kadi nyekundu sababu ya mchezo mbaya. Inter Milan ilishinda Benfica 1-0, nayo Bayern walipata ushindi wa karibu wa 2-1 dhidi ya Copenhagen. Mechi ya PSV na Sevilla ilitoka sare ya mabao mawili. Jude Bellingham alifungia tena Madrid na kuisaidia kuipiku Napoli ya Italia 3-2.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top