TUMBIRI BWALONI
Na Mariita Joshua Ongoro Nimefika kwenye bwalo, nipo foleni nawaona wanachuo kila mtu kashika hamsini zake. Nina mkoba wangu wa ngozi umening’inia begani na kila ninapotembea, mkoba nao unacheza densi ya shwii shwaa. Mwanangu nakumbuka kipindi kile nilikuwa shule ya msingi kijijini Gusii; Mabonde na milima, nilishuka na kupanda nikiwa na kijikoba cheusi chenye mkanda […]