Na Ashley Mbashu
Kulingana na taarifa za hali ya anga, sehemu tajika za kaunti ya Mombasa zimeshuhudia mvua ya mno.
Mafuriko yanaendelea kuzua misukosuko mjini Mombasa. Baadhi ya mikoa iliyoathirika kupita kiasi ni eneo la Bamburi, Old Town na kwingineko.
Takwimu za serikali zinaarifu kuwa kaunti 33 zimeathirika kutokana na mvua kubwa
Idadi ya vifo yasemekana kufika watu sitini na mmoja, wanane hawajulikani waliko,waliojeruhiwa 235 kutokana na mvua hiyo. Nyumba zilizoathirika ni 80518, biashara 143, vituo vya afya 25, vituo vya mifugo 11610,shule 10. Miongoni mwa walioripotiwa kupotea ni maafisa wawili wa halmashauri utozaji ushuru KRA, gari lao kusombwa na maji eneo la Ramisi katika Lungalunga walipokuwa wakisafiri kuelekea Mombasa.
Serikali za kaunti zashauri walio maeneo hatari kuhamia maeneo salama. Hamasisho latolewa wenye magari kuwa waangalifu zaidi.